Mwanzoni mwa mwaka huu (2015) mrembo na muigizaji wa filamu,
Elizabeth “Lulu” Michael aliwa-surprise watu wengi pale alipomzawadia mama yake
nyumba aliyojenga Kimara, jijini Dar es- Salaam.
Je Lulu aliwezaje kufanya mambo makubwa kama hayo katika umri mdogo na kwa
kipato cha kuigiza peke yake? Hayo ni maswali ambayo wengi walijiuliza, kiasi
cha kuwafanya wengine waamini kuwa labda amehongwa.
Lulu
amesema kuwa nyumba hiyo alianza kuijenga kidogo kidogo miaka minne iliyopita
kwa kile alichokuwa anakipata kupitia kazi yake ya uigizaji, lakini watu wengi
hawakufahamu mpaka siku alipoitoa kama zawadi kwa mama yake.
“Kiukweli ile nyumba nimeanza kujenga nikiwa bado mdogo sana, ni nyumba ya chini ya kawaida lakini nilikuwa najenga kidogo kidogo, kwamba leo nikipata laki nampa mama leo kaongezee hiki…kwahiyo ni kwasababu mtu hajui atashangaa Lulu kapata wapi hela za vuuup, lakini ni kitu ambacho kimeenda kidogo kidogo imechukua hata miaka minne..kwahiyo mtu atashtuka kwasababu ameiskia leo sasa ndo hivyo mtu ataanza kusema kahongwa hajui background.” alisema Lulu kupitia The Sporah Show.

0 comments:
Post a Comment