Utata mpya umeibuka
mtoto wa Diamond Utata mpya umeibuka wakati mama kijacho wa staa wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,
akitarajiwa kujifungua muda wowote kutoka sasa, ishu ni juu ya uraia wa mtoto
atakayezaliwa. Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia hiyo zilidai kwamba,
utata umezidi kuigubika familia hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ndugu wa pande
zote kuendelea kuvutana juu ya Zari ajifungulie nchi gani kati ya Tanzania,
Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’. Utata huo umevuja wakati paparazi wetu akiwa
katika mishemishe za kutaka kujua Zari alipo kwa sasa na atajifungulia katika
hospitali ipi ndipo alipopenyezewa ‘ubuyu’ kwamba hadi sasa kuna utata mkubwa
katika familia hiyo. Chanzo kilimweleza mwanahabari wetu kuwa, kikubwa ni
mabishano ya uraia na sehemu sahihi ya kujifungulia mtoto huyo. Kilidai kwamba,
suala hilo limekuja kufuatia ndugu wa Zari kutaka ajifungulie Sauz jambo ambalo
Diamond na familia yake wamekuwa wakilipinga vikali. Ilisemekana kwamba, kwa
upande wake Zari amekuwa njia panda kutokana na shinikizo hilo huku mama
Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye akisisitiza kuwa lazima Zari ajifungulie
Bongo ili amuhudumie mkwe wake huyo. “Yaani ndugu wa Zari wanampa Diamond
wakati mgumu sana kutokana na kuendelea kung’ang’ania Zari akajifungulie kwao
(Sauz ambako kuna ndugu wengi) wakati furaha ya Diamond ni kuona mtoto
akizaliwa Bongo. “Unaambiwa Diamond amechachamaa vibaya, alipoona hawezi
kutumia nguvu ikabidi atumie ushawishi kwa ndugu wa Zari ili wakubali
ajifungulie Bongo lakini wale ndugu wanasema wako tayari kumtumia hata ndege
kwa sababu yupo Bongo, arudi Sauz ambako kuna daktari wao wa familia. Paparazi
wetu baada ya kunyaka utata huo alimtafuta laivu Diamond kwa kujiridhisha zaidi
juu ya hilo ambapo baada ya kumpata alifunguka kwamba, kipindi hiki kuna mambo
kibao yanaibuka kila kukicha jambo linalomshangaza. Alisema kuwa utata huo
alishamalizana nao ndiyo maana hadi muda huu Zari yupo Dar kwa ajili ya
kujifungua. “Ninachoweza kusema kwenye maisha ya kawaida huwezi kuwazuia watu
kuongea jambo wanaloliwaza wao. “Hayo mambo ya utata nimeshayamaliza ndiyo
maana kwa sasa Zari yupo White House (nyumbani kwa Diamond, Tegeta-Madale
jijini Dar) akisubiria saa ya kujifungua. “Kwangu namuomba Mungu ajifungue
salama maana mtoto ni miongoni mwa vitu nilivyotamani kitambo,” alisema Diamond
huku akiwashukuru Watanzania wote wanaoendelea kumuunga mkono kwenye muziki
wake.








0 comments:
Post a Comment